Kamati ya Seneti kuchunguza kiini cha uhaba wa maji

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Lucy Kilalo

KAMATI ya Ardhi na Mazingira ya Seneti inalenga kubainisha chanzo cha bwawa la Ndakaini kukosa maji ilhali mvua kubwa inaendelea kunyesha kote nchini.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Seneta wa Nyandarua, Mwangi Githiomi aliambia wanahabari jana kuwa kamati hiyo itazuru bwawa hilo lililopo Kaunti ya Murang’a, na ambalo ni moja wapo ya yale yanayotegemewa na wakazi wa Nairobi kuwapatia maji.

“Tunataka kujua kwa nini kiwango cha maji katika Bwawa la Ndakaini hakiongezeki ilhali kuna mvua katika eneo hilo,” alisema.

Juma lililopita, Wizara ya Maji iliunda jopo kazi la kuchunguza usimamizi wa bwawa hilo.katibu wa Maji, Bw Joseph Irungu alisema kuwa jopo hilo lina miezi miwili kuwasilisha ripoti yake.

Kamati hiyo ya seneti inalenga pia kubainisha sababu inayofanya bwawa hilo kutojaa maji, suala ambalo limeibua maswali mengi pia miongoni mwa Wakenya.

Wakazi wengi wa Nairobi wamekuwa wakilazimika kununua maji kwa sababu ya bidhaa hiyo muhimu kuwa adimu, hali ambayo pia imehatarisha afya ya wengi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.