12,000 kujiunga na vyuo vya ualimu

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na DERICK LUVEGA

WANAFUNZI 12,000 waliofanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE) mwaka jana, watapata fursa ya kujiunga na vyuo vya ualimu baadaye mwaka huu.

Waziri wa Elimu, Bi Amina Mohamed, alisema idadi hiyo iliongezeka kwa 1,566 ikilinganishwa na wanafunzi 10,434 walioteuliwa mwaka jana.

Vyuo vya mafunzo ya ualimu vinatarajiwa kutoa barua za uteuzi kwa waliohitimu kuanzia Agosti.

Miongoni mwa mambo muhimu ambayo wanafunzi wa vyuo vya walimu watatarajiwa kujifunza ni kuhusu mfumo mpya wa elimu ambao umeanza kutekelezwa katika shule za chekechea.

Akizungumza jana wakati wa hafla ya 86 ya kufuzu katika Chuo cha Mafunzo ya Ualimu cha Kaimosi, Bi Mohamed aliongeza kuwa serikali iko katika harakati ya kumaliza vyeti vya P1.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.