Matayarisho ya Madaraka Dei yapamba moto

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na David Muchui

MATAYARISHO yameshika kasi kuadhimisha Sikukuu ya Madaraka Juni 1 itakayoandaliwa rasmi mjini Meru.

Maafisa wa kikosi cha jeshi na kile cha polisi wameanza mazoezi kuelekea sikukuu hiyo ya kitaifa itakayofanyika katika uwanja wa Kinoru.

Kampuni iliyopewa kandarasi ya kukarabati uwanja huo iko mbioni kutengeneza maeneo ya kuketi, kupanda nyasi, kujenga ua miongoni mwa shughuli zingine za ujenzi kabla tarehe hiyo.

Wanakandarasi wengine wanaendelea na shughuli ya kukarabati makazi ya Kamishna wa Kaunti ya Meru ambako ndiko maankuli ya mchana yataandaliwa kwa wageni waheshimiwa akiwemo Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.