Mshinde katika kiti cha useneta akosoa majaji kwa uamuzi

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Philip Muyanga

JAJI angekubali kuhesabiwa kwa kura wakati wa kusikizwa kwa kesi ya uchaguzi iliyokuwa inapinga kuchaguliwa kwa seneta wa Lamu Anuar Loitiptip, mahakama ya rufaa imeambiwa.

Bw Albeity Hassan Abdalla ambaye kesi yake ya kupinga kuchaguliwa kwa Bw Loitiptip ilitupwa na Mahakama Kuu, aliwaambia majaji wa mahakama ya rufaa Alnashir Visram, Wanjiru Karanja na Martha Koome ya kuwa kulikuwa na sababu za kutosha za kulazimu kuhesabiwa tena kwa kura.

Kupitia wakili Yusuf Abubakar, Bw Abdalla anasema jaji Asenath Ongeri alikosea alipokosa kuchanganua ushahidi uliokuwa mbele yake, ndiposa akafikia uamuzi wa kimakosa.

“Jaji alikosea kwa kutofutilia mbali matokeo ya maeneo bunge ya Lamu Mashariki na Magharibi,” akasema Abubakar.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.