Wakulima wasuta wabunge wa Rift Valley kuwapuuza

Taifa Leo - - Riziki - Na Titus Ominde

WABUNGE wa Kaskazini mwa bonde la ufa wamelaumiwa kwa kupuuza masaibu ya wakulima.

Kwenye mkutano na wanahabari mjini Eldoret jana, wakulima walisema wabunge wengi kutoka eneo hilo wamefumbia macho masaibu ambayo yamekumba wakulima husika.

Miongoni mwa maslahi hayo ni kucheleweshwa kwa malipo ya nafaka baada ya kuwasilisha nafaka hiyo kwa bodi ya NCPB, viwavi jeshi na hata uhaba wa pembejeo za kilimo.

Lakini walimsifu mbunge wa Moiben, Bw Sila Tiren, kwa kujitolea mhanga kupigania haki na maslahi ya wakulima.

“Uasin Gishu ina wabunge sita, lakini ni mbunge wa Moiben pekee anayepigania wakulima, Wabunge wengine wako wapi?” akauliza mkulima James Malakwen.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.