Wakulima wa mahindi wadai NCPB Sh250m

Taifa Leo - - Riziki - Na Osborn Manyengo

WAKULIMA wa Mahindi Kaunti ya Trans-nzoia wanadai zaidi ya Sh250 milioni kutokana na mahindi waliyowasilisha katika Bohari la Kitaifa la mazao Nafaka NCPB tanu Novemba mwaka jana.

Akiongea na wanahabari mjini Kitale, gavana Patrick Khaemba aliitaka serikali kuu kupitia wizara ya Kilimo kuharakisha malipo hayo.

Alieleza kuwa wakulima walivuna mahindi kidogo kutokana na kushambuliwa na viwavi.

“Kwa nini wakulima waliouza mahindi kidogo waliyovuna hawajalipwa hadi sasa? Tayari kuna viwavi katika mashamba na wakulima hao wanahitaji pesa ili kununua dawa ya kuvikabili,” akasema.

Bw Khaemba pia aliomba serikali yake isaidiwe kupata dawa na kukabiliana na wadudu hao hatari, aliosema huangamiza ekari za mashamba ya mahindi kwa muda mfupi mno.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.