Familia yalaumu hospitali kwa kifo cha mtoto baada ya kuzaliwa

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na DENNIS LUBANGA

FAMILIA kutoka kijiji cha Kapsokwony katika eneobunge la Mlima Elgon, Kaunti ya Bungoma, imetishia kushtaki Hospitali ya Kory Family kutokana na madai ya kuzembea na kusababisha kifo cha mtoto wao alipokuwa akizaliwa.

Bw George Chesebe alisema wauguzi wa hospitali hiyo tawi la Kimilili walizembea na kusababisha kifo cha mtoto wao mnamo Jumapili asubuhi.

“Wauguzi waliohudumia mke wangu hawakuwa na ujuzi wowote. Daktari wa zamu aliniambia mke wangu alifaa kufanyiwa upasuaji ilhali mimi sikupewa stakabadhi zozote kutia saini,” akasema Bw Chesebe.

Bi Virginia Ngeywo, 24, mkewe Bw Chesebe, alishutumu daktari wa zamu kwa kuchangia katika kifo cha mtoto wake.

Afisa Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt Allan Kundu alikanusha madai hayo akisema wana madaktari waliohitimu na walijaribu kila mbinu kusaidia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.