Mahakama yatupa rufaa ya watatu katika kesi dhidi ya Mvurya

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na PHILIP MUYANGA

GAVANA wa Kwale Salim Mvurya jana alipata afueni Mahakama ya rufaa ilipotupilia mbali ombi la wakazi watatu wa Kwale waliotaka kubadilishwa na kuwa wakata rufaa katika kesi iyayopinga uamuzi wa mahakama kuu wa kuthibitisha kuchaguliwa kwake.

Majaji wa mahakama ya rufaa Alnashir Visram, Wanjiru Karanja na Martha Koome walitupilia mbali rufaa hiyo iliyokuwa imewekwa na Bw Mwamlole Tchapu Mbwana kutoka kwa orodha ya kesi za rufaa za uchaguzi ambazo hazikuwa zimemalizwa kusikizwa.

Katika uamuzi wao, majaji hao watatu walisema kuwa hakuna sheria inathibitisha uhalali wa ombi la Suleiman Warrakah, Mwarapayo Mohamed na Matsudzo Mwamrezi la kubadilishwa kama wakata rufaa badala ya Bw Mbwana.

Majaji hao walisema kuwa hawawezi kutoa sheria za mahakama kuu ambazo zinaruhusu kubadilishwa kwa mweka kesi na kuzitumia katika mahakama ya rufaa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.