Usafirishaji takataka kwa mikokoteni wapigwa marufuku

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti -

SERIKALI ya Kaunti ya Mombasa imepiga marufuku usafirishaji na umwagaji taka kwa mikokoteni katika jaa la Kibarani huku mpango wa kuhamisha jaa hilo ukishika kasi.

Wasafirishaji wa taka kwa kutumia mikokoteni wamekuwa wakihatarisha maisha yao wakisafirisha taka hizo kutoka mitaani hadi Kibarani wakipitia barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi.

Maafisa wa mazingira wa kaunti hiyo walisema jaa hilo litahamishwa hadi Mwakirunge ifikapo Juni.

Msimamizi mkuu wa mawasiliano katika kaunti hiyo Richard Chacha aliiambia Taifa Leo kuwa malori 12 ya kusafirisha taka kutoka mitaani hadi katika jaa yamenunuliwa.

Bw Chacha alisema eneo la Kibarani litasafishwa na taka zote kupelekwa katika jaa Mwakirunge.

Awali Gavana Hassan Joho alisema jaa la Kibarani linaipatia kaunti yake, ambayo ni kivutio kikuu cha utalii, picha mbaya na akaagiza kufungwa kwake kufikia mwishoni mwa mwezi wa Juni

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.