Wakazi waandamana kulalakimia huduma duni za Kenya Power

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti -

WAKAZI wa mji wa Kapenguria waliandamana jana kulalamikia kile walichosema ni huduma mbovu za kampuni ya kusambaza umeme ya Kenya Power.

Wakibeba matawi na mabango yenye maandishi ya kukashfu kupotea kwa stima mara kwa mara, waandamanaji hao walifika kwenye ofisi ya Kenya Power mjini humo na kuketi chini mlangoni wakilalamikia kupotea kwa stima kwa mwezi wa pili sasa.

Wakiongozwa na MCA maalum Bw Elijah Kaseuseu na mwenzake wa Mnagei, Bw Benjamin Araule, waliipa Kenya Power siku tano imhamishe meneja wa tawi la kaunti hiyo, Bw Milimo Amusavu.

“Mlingoti wa stima ulianguka kwenye lango la shule ya Kamol na unahatarisha maisha. Ni wiki ya tatu na hakuna hatua iliyochukuliwa,” akasema Bw Kaseuseu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.