Wakazi wapinga Sh50m kujenga makao ya gavana

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti -

WAKAZI wa Kaunti ya Busia wamepinga pendekezo la kutumia Sh50 milioni kujenga makao ya gavana wao.

Pingamizi hizo ziliibuka jana kwenye kikao cha kusikiza maoni kuhusu makadirio ya bajeti ya 2018/19 Busia kilichoandaliwa katika eneobunge la Budalangi.

Wakiongozwa na David Munyolo na Alphonse Otiato, wakazi hao walitaka kikao hicho kilichoongozwa na diwani wa Chakol Kaskazini, Julius Etiang, kupunguza pesa zilizotengewa mradi huo hadi Sh25 milioni, huku nusu iliyosalia ikielekezwa kwa miradi muhimu katika wadi zote 35.

Walishangaa kuwa tangu mfumo wa ugatuzi uanzishwe nchini mradi huo umekuwa ukitengewa pesa pasipo lolote kutekelezwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.