Kampuni yawasaidia vijana waliobadilika

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti -

KAMPUNI ya mbegu ya Kenya Seed imetoa mbegu ya zaidi ya Sh200,000 kwa vijana wa Kerio Valley walioacha uhalifu .

Akizindua mpango huo mjini Kitale, Mkurugenzi Mkuu, Bw Azaraias Soi alisema wameonelea ni vyema kuwapa vijana hao mbegu ili wajishughulishe na kilimo badala ya kujiingiza katika uhalifu.

Vijana hao waliokuwa wakitenda uhalifu mpakani mwa jamii za Pokot na Marakwet walisalimisha silaha zao na kuamua kufanya kazi ya kilimo.

“Tunajua usalama ukikosekana hata nasi hatuwezi kuwa na amani,” akasema Bw Soi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.