Mshukiwa wa unajisi huru kwa bondi Sh200,000

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Kalume Kazungu

MAHAKAMA ya Lamu imemwachilia kwa dhamana ya Sh200,000 mshukiwa aliyemnajisi msichana wa miaka minne.

Abdulaziz Abubakar Kanda,50, alishtakiwa kwamba mnamo Mei 9 mwaka huu, majira ya saa saba mchana, alitenda kosa hilo katika mtaa wa Riyadha, lokesheni ya Langoni, Kaunti Ndogo ya Lamu Magharibi. Mshukiwa anadaiwa kumbembeleza mtoto huyo kwa peremende kabla ya kumuingiza chumbani mwake na kumnajisi.

Aidha mshukiwa alikana kutekeleza kosa hilo, hivyo kuachiliwa kwa dhamana.

Kesi hiyo itasikilizwa mnamo Julai 12 mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.