DPP: Mwanablogu Cyprian Nyakundi asiendelee kuzuiliwa

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Benson Matheka

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP), Noordin Haji, ameagiza mwanablogu Cyprian Nyakundi aliyekamatwa siku sita zilizopita nje ya Mahakama ya Milimani Nairobi asishtakiwe.

Kwenye barua kwa maafisa wa ofisi yake Kaunti ya Kiambu ambapo polisi waliwasilisha ombi wakitaka waruhusiwe kuendelea kumzuilia Bw Nyakundi, Bw Haji alisema makosa anayodaiwa kutenda na ambayo polisi wanadai wanachunguza, ni madogo sana na mtu hafai kuzuiliwa kwa zaidi ya siku tatu.

“Nimegundua kwamba makosa yanayochunguzwa kuhusiana na ombi hilo ni madogo na yanahusiana na mtandao na mtu hafai kuzuiliwa kwa zaidi ya siku tatu,” alisema Bw Haji kwenye barua aliyotuma nakala kwa wakili Apollo Mboya.

Alimuagiza afisa anayesimamia ofisi ya mashtaka kaunti ya Kiambu kuondoa ombi la polisi kortini na kufunga faili yake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.