Wawili washtakiwa kunaswa na pembe za Sh3.2 milioni

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Pius Maundu

WANAUME wawili walishtakiwa jana katika Mahakama ya Makindu, Kaunti ya Makueni kwa kupatikana na pembe za ndovu za thamani ya Sh3.2 milioni.

Bw David Mutua na Bw Wambua Muia walikamatwa na maafisa wa Shirika la kulinda wanyama pori (KWS) wakiwa mjini Emali.

Maafisa hao walijifanya wateja wa pembe hizo baada ya kupashwa habari na umma kwa washukiwa walikuwa na bidhaa za wanyama pori kinyume cha sheria.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.