Balozi wa Israeli Uturuki afurushwa

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

BALOZI wa Israeli nchni Uturuki jana alifurushwa kutoka taifa hilo kufuatia mzozo uliosababishwa na mauaji ya Wapalestina yaliyotekelezwa na Israeli katika eneo la Gaza.

Balozi Eitan Naeh aliondoka kuelekea Tel Aviv kupitia uwanja wa ndege wa

Tel Aviv huku akimulikwa na kamera za wanahabari, ambao, ilidaiwa, walialikwa kurekodi kuondoka kwake.

Awali taifa la Uturuki nalo lilikuwa limemwagiza balozi wake nchini Israeli kurejea nyumbani “kwa mashauriano.

Jana, Wizara ya Masuala ya Kigeni ilisema kuwa balozi wa Israeli aliamriwa kuondoka nchini Uturuki “kwa muda mfupi.”

Israel ilikasirishwa na kile ambacho ilitaja kama kudhulumiwa kwa balozi wake, nchini Uturuki huki ikiapa kuliza kisasa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.