Lofa akesha mangweni kumhepa dadake mkali

Taifa Leo - - Dondoo! Za Hapa Na Pale - Na Nicholas Cheruiyot

MLOFA wa hapa aliamua kukesha kwa mama pima alipoarifiwa kwamba dadake mkali alikuwa amefika kwake kumtembelea.

Udaku uliofika mezani yetu unaarifu kuwa mlofa alikuwa akisaidiwa na dada yake kuwalipia watoto wake karo kwa sababu jamaa amezama kwa pombe.

Juzi, aliamua kumtembelea ndugu yake bila taarifa. Jioni ya siku hiyo, mlofa aliwaaga walevi akitaka kwenda kwake lakini mmoja wao akampasha habari zilizomtia baridi. Aliambiwa dadake alionekana akishuka kwa gari na kufululiza hadi kwake.

“Sina ujasiri wa kusimama mbele yake kabisa. Najua atanigombeza vikali. Afadhali nilale papa hapa,” jamaa alilia na kujibwaga chini kwa mama pima.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.