Tabia za kupiga ramli zafanya atemwe na mke

Taifa Leo - - Dondoo! Za Hapa Na Pale - Na Holiness Mwambi

KALAMENI aliyekuwa akifanya kazi ya mlinda lango eneo hili alibaki kapera baada ya kuachwa na mke alipoingilia kazi ya uganga.

Penyenye zinasema kuwa kalameni alishawishiwa na marafiki zake kuwa kazi ya uganga ina mapato mazuri kuliko ubawabu.

“Wachana na kazi ya kujitesa na mambo ya kulala nje kila ukipigwa na baridi tena ni hatari waweza kushambuliwa na wezi ilhali ina mshahara duni sana,” marafiki zake walimshauri. Kalameni kusikia hivyo, aliamua kuachana na kazi ya askari gongo na akaingilia uganga.

Mkewe alimshauri kuachana na kazi hiyo akimwambia ameokoka na hataki ushirikina katika nyumba yao. Jamaa alipokataa kuacha kupiga ramli, mkewe aliamua kuondoka na kuanza maisha kivyake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.