Adhabu ya kufyeka nyasi kwa kuchafua ukuta

Taifa Leo - - Dondoo! Za Hapa Na Pale - Na Richard Maosi

KALAMENI kutoka mtaani hapa alilazimika kufyeka uwanja kama adhabu ya kuchafua ukuta wa nyumba ya mdosi wake kwa mkojo.

Penyenye zinaarifu jamaa alikuwa akifanya kazi kwa bidii hadi alipoamua kuzima haja katika ukuta wa mwajiri wake. Kwa bahati mbaya, mdosi wake alimuona na akaamua kumwadhibu.

“Ili iwe funzo kwake, mdosi alisubiri jamaa amalize haja yake, kisha akamkabidhi upanga wa kufyeka nyasi na maji ya kunywa katika chupa na kumuagiza akate nyasi katika uwanja uliozunguka boma lau sivyo amwage unga,’’ alisimulia mpambe wetu.

Jamaa aliapa kutorudia kosa baada ya kumwaga jasho siku nzima akifyeka nyasi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.