Gor matumaini sufufu watafuzu 8-bora CAF

K’ogalo imezoa alama 2 kutokana na mechi mbili, alama 2 nyuma ya Alger

Taifa Leo - - Mawaidha Ya Kiislamu - Na JOHN ASHIHUNDU

Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr amesema timu yake ina uwezo wa kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi lao la michuano ya CAF Confederations Cup, na kutinga robo fainali.

Mabingwa hao mara 16 wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) wametoka sare katika mechi mbili za kwanza dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na USM Alger ya Algeria, nas asa wako nyuma ya USM wanaoongoza kwa pointi nne.

Timu mbili zitafuzu kutoka kila kundi, lakini Kerr amewataka wachezaji wake walenge kumaliza katika nafasi ya kwanza.

“Tunapaswa kuamini tunaweza kuibuka washindi wa kundi hili,” kocha huyo alisema jana baada ya vijana wake kucheza na USM, Jumatano usiku. Tumebakisha maechi nne, mbili hapa nyumbani na mbili ugenini. Tunaweza kutimiza ndoto yetu iwapo tutaendelea kupigana kwa bidii,” aliongeza.

Yanga ya Tanzania na Rayon ambazo pia zimo kwenye kundi hilo, ziliagana kwa sare ya 0-0 mjini Dar es Salam, pia Jumatano usiku. Hii ilikuwa mara ya nane kwa Yanga kuondoka uwanjani bila ushindi tangu mwezi Aprili.

Katika mechi hizo, klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania imetoka sare mara tatu na kushindwa mara tano.

Matokeo yao dhidi ya Rayon yamewaacha Yanga katika nafasi ya mwishoni katika kundi hilo, kwa pointi moja baada ya kubwagwa 4-0 na USM Alger katika mechi ya kwanza.

Kwenye mechi yao dhidi ya Rayon Sports, miamba hao wa Jangwani walicheza kwa kiwango cha chini, huku nafasi yao ya wazsi pekee ikipatikana dakika ya 68, kombora la Obrey Chirwa lilipogonga mwamba na kutoka nje. Mbali na jaribio hilo, Yanga walicheza vibaya, huku wakishindwa kuelewana uwanjani.

Wakati mashambuliaji yakiongozwa na Chirwa, safu ya ushambuliaji ilishindwa kung’ara.

Walicheza mechi hiyo bila nyota Ibrahim Ajib na Papy Tshishimbi ambao pia hawakucheza mechi ya kwanza dhidi ya USM Alger.

Mwamuzi, Helder Martin kutoka Angola alilaumiwa na Rayon Sports kwa kukataa mabao yao mawili akidai wafungaji walikuwa wameotea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.