Mibabe ya raga kwa shule za sekondari kujulikana leo

Taifa Leo - - Mawaidha Ya Kiislamu - Na GAITANO PESSA

BINGWA wa fainali ya raga ya wachezaji saba kila upande ya 2018 Maseno Sevens chini ya udhamini wa gazeti la Mwanaspoti atabainika leo, wenyeji Chavakali watakapokwaruzana na miamba wa mchezo huo katika Shule ya Upili ya Maseno School.

Mibabe hao wawili walifika fainali ya dimba hilo Jumapili iliyopita baada ya kuwazidi wapinzani Ambira na Kakamega High katika mechi kali ya nusu fainali katika Shule ya Upili ya Maseno.

Hata hivyo, mvua kubwa ilikatiza makala hayo na kuwalazimu waandalizi kusongesha mechi ya mwisho hadi leo katika Shule ya Upili ya Chavakali, hii ikiwa na maana kuwa Maseno watashiriki mechi hiyo bila shangwe za wafuasi wao sugu.

Katika kabiliano hilo la nusu fainali ya kwanza, John Baraka na Barnabas Osoro wa Maseno walitia kimiani miguso yao katika kipindi cha kwanza na cha pili mtawalia naye Walter Omanyo akafunga mikwaju yote miwili na kuipa Maseno alama 14-0 dhidi ya Ambira. Katika mechi ya pili, Chavakali iliwapepepta Kakamega 12-10 na kujikatia tiketi ya fainali.

Kocha wa Maseno, mabingwa wa kitaifa 2014 Paul Nyamita alisema wanatumia fainali ya leo kujiandaa kwa mashindano yajayo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.