Idadi ya timu za kimia barani yahatarisha nafasi ya Kenya

Taifa Leo - - Mawaidha Ya Kiislamu - Na JOHN KIMWERE

KENYA ina matumaini finyu ya kuandaa ngarambe ya bara Afrika mwaka huu katika voliboli ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20.

Hatua ya kuongezwa kwa idadi ya timu zitakazoshiriki kufikia 24 kutoka 12 itaifanya Kenya kuponyokwa na haki za kuandaa kipute hicho.

Katibu wa Shirikisho la Voliboli la Kenya (KVF), Ben Juma amesema kukosekana kwa kumbi za ndani za hadhi ya kimataifa ndilo tatizo kuu.

“Kenya tuna ukumbi mmoja wa Kasarani Indoor Arena ambao una uwezo wa kutumiwa na timu 12 pekee,’’ alisema na kuongeza kuwa endapo zaidi ya nchi 12 zitathibitisha kushiriki pambano hilo bila shaka Kenya itaikosa nafasi hiyo.

Aliongeza ‘’Kulingana na mwongozo wa FIVB shindano linalohusisha zaidi ya timu 12 linahitaji zaidi ya kumbi mbili za ndani kwa ndani zinazotimiza hadhi ya kimataifa lakini Kenya inajivunia ukumbi huo mmoja.’’ Kipute cha mwaka huu kimeratibiwa kufanyika Agosti, 17 hadi 26.

Kadhalika katibu huyo anazitaka serikali za Kaunti nchini kujenga viwanja vya michezo ya ndani bila kusubiria serikali ya kitaifa.

Anazishauri kuwa kuwepo kwa viwanja hivyo kutachangia serikali hizo kufaidi pakubwa kwa kuzikodisha. Vilevile alisema mafanikio hayo yatawapa wachezaji chipukizi nafasi bora kukuza talanta zao wangali katika umri mndogo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.