Mechi zote za kabumbu ya FKF zasitishwa kupisha mfungo wa Ramadhan

Taifa Leo - - Mawaidha Ya Kiislamu - Na ABDULRAHMAN SHERIFF

MECHI zote za ligi na mashindano yanayotayarishwa na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) tawi la Pwani Kusini zimesimamishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa sababu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Afisa Mkuu wa tawi hilo, Sumba Bwire alisema wamesimamisha ili kuwapa Waislamu kutimiza nguzo mojawapo ya dini yao ya kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akitangaza kuahirishwa kwa mechi hizo, Ofisa Mkuu wa FKF Pwani Sumba Bwire alisema imekuwa ni kawaida miaka na mikaka kwa ligi na mashindano yote ya soka kuahirishwa mkoani Pwani wakati wa kipindi hicho cha Ramadhani.

“Tunatangaza rasmi kuwa hakutakuwa na mechi zozote zetu kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa ajili ya kuwapa fursa wachezaji, maafisa wa klabu, waamuzi na viongozi wa FKF wa kutimiza nguzo yao hiyo muhimu ya dini ya Kiislamu,” akasema Bwire.

Alisema mechi zinatarajiwa kuanza tena Juni 23, itakuwa wiki moja baada ya Waislamu kukamilisha mfungo wao wa siku 29.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.