Sanchez kutegemea kismati yake katika taji la FA fainali kesho

Taifa Leo - - Spoti -

ALEXIS Sanchez atatua uwanjani Wembley kwa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea kesho akitumai kismati chake kwenye shindano hili kitamsaidia kuridhisha mashabiki wa Manchester United.

Sanchez alijiunga na United mwezi Januari kwa kandarasi ya miaka minne na nusu, ambayo ripoti zilisema ni ya kudondosha mate kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Mchile huyu amekuwa akifanya vyema sana katika kombe hili. Ilikuwa sherehe kubwa Sanchez aliposajiliwa na Jose Mourinho kutoka Arsenal katikati ya msimu hasa baada ya United kushinda mahasimu na majirani Manchester City katika vita vya kupata huduma zake. Hata hivyo, Sanchez hajaridhisha. Amepachika mabao matatu pekee katika mechi 17.

Bao muhimu sana alifungia United ni la kusawazisha katika mechi ya nusu-fainali ya Kombe la FA mwezi uliopita ambapo vijana wa Mourinho walilemea Tottenham 2-1. Itakuwa fainali yake ya tatu ya Kombe la FA katika misimu minne nchini Uingereza.

Sanchez alicheka na nyavu katika fainali na mwaka 2015 na 2017 na kusaidia Arsenal kuibuka bingwa kwa kupiga Aston Villa 4-0 na Chelsea 2-1, mtawalia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.