Klinsmann adai angeletea USA tiketi ya Urusi’18

Taifa Leo - - Spoti -

KOCHA wa zamani wa Marekani, Jurgen Klinsmann anaamini angeongoza timu hiyo kuingia Kombe la Dunia nchini Urusi kama hangepigwa kalamu wakati wa mechi za kufuzu.

Katika mahojiano na gazeti la Sports Illustrated, mvamizi huyu wa zamani wa Ujerumani na kocha alishikilia kwamba angefaulu kubadili matokeo ya timu hiyo katika kampeni ya kufuzu kabla ya kutemwa mwaka 2016.

Klinsmann alimwaga unga baada ya Marekani kufungua kampeni yake kwa vichapo dhidi ya Mexico 2-1 na Costa Rica 4-0 katika raundi ya mwisho ya mchujo wa Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean (CONCACAF), ambayo inaleta pamoja mataifa sita.

Nafasi yake ilitwaliwa na Muamerika Bruce Arena, lakini safari ya timu hiyo kufika Urusi ikazimwa ilipobwagwa na Trinidad & Tobago 2-1 katika mechi ya mwisho.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.