GOR MAHIA WAAMINI WATAINGIA 8ÙBORA CAF

Taifa Leo - - Spoti - LYON, Ufaransa

ANTOINE Griezmann alikuwa shujaa wa Atletico Madrid baada ya kuifungia mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Marseille na kuisaidia kushinda Ligi ya Uropa kwa mara ya tatu katika misimu tisa.

Ni taji la kwanza kubwa kwa Griezmann akivalia jezi ya Atletico, na njia nzuri ya kuaga mashabiki wa Atletico ikiwa atanyakuliwa na Barcelona jinsi fununu zinavyozidi kusema.

Griezmann, ambaye alilelewa mjini Macon, kilomita 70 kutoka Lyon, alifungia Atletico bao moja katika kila kipindi, bao la pili baada ya Marseille kupata pigo, nahodha wake Dimitri Payet alipoumia. Payet huenda akakosa Kombe la Dunia nchini Urusi mwezi ujao.

Griezmann sasa amefunga mabao 29 msimu huu, ingawa bao la mwisho kutoka kwa Gabi ndilo lililohakikishia Atletico ushindi.

“Hii ni zawadi muhimu kwangu

baada ya kuondoka nyumbani nikiwa na umri wa miaka 14, kwa bidii nilizoweka, wakati mgumu niliopitia,” alisema kabla ya Jumatano. Griezmann ambaye maisha yake yote ametandaza soka nchini Uhispania, alijivunia taji moja pekee la shindano la Super Cup la Uhispania.

Ufanisi wa Atletico uliwasili baada ya masikitiko ya kulimwa na Real Madrid katika fainali za Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2014 na 2016. Atletico iliwahi kushinda Ligi ya Uropa mwaka 2010 na tena 2012, taji la pili likipatikana miezi sita pekee baada ya Diego Simeone kuteuliwa kuongoza timu hii.

Simeone, ambaye alilazimika kutazama mechi katika sehemu ya mashabiki kutokana na kupigwa marufuku kuwa katika kisanduku cha makocha, alisema ushindi huo ni zawadi ya bidii ya vijana wake na hata akasalia mwingi wa matumaini Griezmann huenda akashawishika kusalia Atletico.

Marseille ilikuwa na hamu kubwa ya kushinda taji la pili la Bara Ulaya katika historia yake, kwenye ardhi ya Ufaransa, miaka 25 tangu ilime AC Milan 1-0 katika fainali ya makala ya kwanza ya Klabu Bingwa.

Licha ya mashabiki wengi kujitokeza kuipa Marseille motisha, wenyeji walikosa makali. Hali hii ilichangia mashabiki kuanza kutisha kuvuruga mechi pale walipowasha fataki mwisho wa upande mmoja wa uwanja, na kuzitupa uwanjani mechi ikielekea kutamatika.

Mechi hata hivyo iliendelea hadi kipenga cha mwisho, huku vijana wa kocha Rudi Garcia wakizidiwa maarifa kabisa.

“Tulipoteza nafasi nzuri katika kipindi cha kwanza. Kwanza, tulikuwa na nafasi nzuri sana ya kuchukua uongozi, na pili, kosa tulilofanya liliipa Atletico bao la ufunguzi,” alisema Garcia.

“Kichapo hiki ni kikubwa, lakini timu bora iliibuka mshindi.”

Atletico ilipigiwa upatu kuzima Marseille iliyoanzia kampeni yake katika raundi ya tatu ya kufuzu Julai mwaka jana.

Kufika fainali ni mafanikio makubwa kwa vijana wa Garcia, ingawa watajilaumu wenyewe kutonyakua taji baada ya kupoteza nafasi kadhaa murwa.

Picha/afp

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone pamoja na familia yake washerehekea taji la UEFA Europa League walilonyakua baada ya kushinda Olympique de Marseille mjini Lyon, Ufaransa mnamo Jumatano.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.