Waburundi debeni rais ahudumu hadi 2034

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

RAIA wa Burundi jana walienda debeni kushiriki kura ya maamuzi kuhusu marekebisho ya Katiba yanayolenga kumwezesha Rais Pierre Nkurunziza kuongoza hadi mwaka wa 2034.

Kura hiyo ya maamuzi inajiri wakati ambapo nchi hiyo imegubikwa kwenye mzozo wa kisiasa uliochochewa na hatua ya Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa watatu mnamo 2015.

Takriban watu 1, 200 wameuawa na wengine 400,000 kuhama katika fujo zilizotokea wafuasi wa upinzani walipokabiliana na maafisa wa usalama katika maandamano na kupinga hatua hiyo.

Jana, mamia ya walirauka mapema kushiriki zoezi hilo ambapo walitakiwa kupiga kura ya “Ndio” au “La” kwa marekebisho hayo ya Katiba.

“Foleni ndefu zilishuhudiwa katika vituo vya kupigia kura jijini Bunjumbura. Rais wa Burundi walikuwa na hamu kubwa kujitokeza kupiga kura,” Msemaji wa Ikulu ya Rais Willy Nyamitwe alisema kwenye ujumbe katika mtandao wa twitter.

Rais Nkurunziza

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.