Nyota

Taifa Leo - - Fumbo & Falaki - Na Sheikh Khabib

KONDOO

Machi 21 – Aprili 20: Hata kama unamchukia namna gani jirani yako katika mtaa unamoishi, jaribu kuondoa chuki hiyo kwani naona anaweza kukufaa kwa mambo mengi. Pia kuna manung’uniko kuhusu uhusiano wako na majirani zako.

NG’OMBE

Aprili 21 – Mei 20: Endelea kuwafaa watu wengine kama ambavyo umekuwa ukifanya wala usitarajie wakulipe kwa wema wako. Dhawabu yako itatoka kwa Mungu kwani anaona kazi nzuri ambayo unafanya.

MAPACHA

Mei 21 – Juni 21: Hii ndiyo siku bora ya kuwatembelea jamaa na marafiki kwani kuna mambo mengi mapya ambayo utayapata kutoka kwao na yakufae kwa namna fulani maishani. Usitumie barabara ya kawaida kwenda nyumbani kwani naona ina mikosi.

KAA

Juni 22 – Julai 22: Kuna mambo ya kibinafsi ambayo yanakusumbua na yameathiri vibaya matokeo katika kazi unayofanya. Muone mtaalamu akusaidie kuyatatua kabla hayajasababisha athari mbaya zaidi.

SIMBA

Julai 23 – Agosti 22: Unajiweza kifedha lakini huna mipango mizuri ya kutumia pesa zako na nyingi zinapotea kwa mambo yasiyo na manufaa kwako wala watu wako. Tafuta ushauri kutoka kwa watu walio karibu nawe ili kubadilisha hali hiyo.

MASHUKE

Agosti 23 – Septemba 23: Furaha imo njiani kutokana na mafanikio yako katika jambo ambalo umejaribu kwa siku nyingi bila kufaulu. Hata hivyo unashauriwa uchunge furaha hiyo isikutie kwenye majaribu ya dunia kwani ni mengi.

MIZANI

Septemba 24 – Oktoba 23: Huu ndio wakati wa kufanya mabadiliko ya maana katika maisha yako baada ya miaka mingi ambayo umeishi bila kujali kuhusu kesho wala kesho kutwa. Kuna uwezekano wa kubadilisha kabisa maisha yako bora tu umakinike.

NGE

Oktoba 24 – Novemba 22: Nyota yako inakushauri uwe kama washirika wako wengine kwa kudumisha furaha kwa wote na ufanye mageuzi yanayohitajika mahali unakofanya kazi. Ujuzi wako wa miaka mingi utakufaa.

MSHALE Novemba 23 – Desemba 21: Umekuwa mvivu wa kutafuta mambo mapya unayohitaji ili kufanikisha maisha yako. Ni lazima ujue kuwa hakuna chochote kizuri kinachopatikana bila kumwaga jasho. Amka sasa ushughulike.

MBUZI

Desemba 22 – Januari 20: Watu walio karibu nawe watakuwa waaminifu na wachangamfu iwapo utawatendea haki. Naona unahitaji msaada fulani kutoka kwao na hutaweza kuupata usipobadilisha msimamo wako kuwahusu.

NDOO

Januari 21 – Februari 19: Ni wakati mwema wa kujaribu mambo yasiyo ya kawaida na kukutana na watu wapya. Huenda utampata mpenzi wa kukuondolea upweke ambao umekuwa nao katika siku za hivi karibuni.

SAMAKI

Februari 20 - Machi 20: Unakaribia kupata msaada ambao unahitaji sana ili kusukuma mbele kazi yako ambayo inaonekana kukwama. Shughulikia suala hilo kwa uwazi na utafaulu. Hakikisha unawakumbuka wahusika wengine ukifanikiwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.