Faida tele za kiroho na kimwili kwa mfungaji

Ndio mwezi wa pekee ambao Allah anatoa rehma kwa waja wake, anawasamehe dhambi na kuwatoa katika moto

Taifa Leo - - Mawaidha Ya Kiislamu - Na HAWA ALI

KILA sifa njema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Sala na salamu zimuendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allahu alaihi wa sallam) na ahli zake na maswahaba wake.

Mwezi wa ramadhani ni katika miezi bora katika miezi kumi na mbili ndani ya mwaka mzima, ndiyo mwezi ambao Allah subhaanahu wataala amebainisha wazi kheri na neema nyingi zilizomo ndani yake, pia ni ibaada ambayo walifanya wema waliopita na hata kaumu zilizopita. Pia ndio mwezi ulioteremshwa Qur-an, ndiyo mwezi waislamu na Mtume swallalahu alyhi wasallam wamepata futuuhat na ufunguzi wa mji wa Makka baada ya kufukuzwa na kuteswa kwa kulingania dini, ndio mwezi wa pekee ambao Allah subhaanahu wataala anatoa rehma kwa waja wake, anawasamehe dhambi na makosa waliofanya pamoja na kuwatoa katika moto na adhabu iumizayo.

Amri ya kufunga saumu inapatikana katika kaumu karibu zote ingawa kanuni zake zimekhitalifiana. Allah (subhanahu wataala) anasema “”Enyi mlioamini, mmelazi-mishwa kufunga Saumu kamawalivyolazimishwa wa kabla yenu ilimpate kumcha Mungu”

Lengo kuu la sisi kuwekewa ibada ya funga ni tupate kumcha Allah. Kifungu hiki cha Maneno kinaeleza hekima kubwa inayofungamana na saumu. Ni desturi ya Qur’an inapotoa amri yenye maana, papo kwa papo inaeleza faida yake ili mtu ajue na atosheke na hekima ya kupewa amri hiyo. Katika kifungu hicho kusudi la Saumu limeelezwakuwa ni kupata Taqwaa, yaani, ucha-mungu. Neno Taq-waa, linatumiwa katika Qur’an kwa maana tatu: (1) Kuepukana na maumivu, (2) kuepukana na dhambi, (3) kufikia utakatifu ulio juu wa mambo ya kiroho.

Kufunga Saumu kunatoa mambo yote hayo matatu. Kwa mara ya kwanza maelezo haya yanaonekana yenye kushangaza, kusema ya kwamba kufunga saumu kunamhifadhi mtu na maumivu, kwani kufunga kwenyewe kunamtia mtu kadiri fulani ya maumivu.

Lakini tukifikiri kidogo tutaona ya kwamba kufunga Saumu kunawafunza watu somo linaloleta manufaa juu ya taifa lao.

(1) Somo la kwanza ni hili ya kwamba, tajiri ambaye hajaona uchungu wa njaa wala kupungukiwa hawezi kutambua tabu za ndugu zake walio maskini ambao mara nyingi wamekaa bila chakula. Lakini yeye mwenyewe anapofunga, anatambua njaa ni kitu gani na anaweza kufikiria yote yanayowasibu maskini. Hivyo anaanza kuwahurumia maskini, na matokeo yatakuwa ni kuongezeka hali njema za taifa zima.

(2) Sababu nyingine ya kufunga ni kuwa uislam hautaki wafuasi wake wawe wazembe na wavivu na wasioelekea kuvumilia tabu. Bali inawataka wawe tayari na wenye uwezo wa kupokea kila namna ya upungufu na shida katika wakati wa tabu. Saumu zinawafanya Waislamu kuwana tabia za kuvumilia njaa na kiu na kujizuia nafsi zao katika mahitaji na shauku, na hao wanaoifuata amri hii kwa uaminifu sana hawawi wavivu kamwe, wala hawawi wenye kujiendekeza.

(3) Tena Saumu inamhifadhi mtu na dhambi, maana dhambi huzalika katika kupenda stareheza kimwili. Mtu anapokuwa amezoea tabia fulani inamuwia shida sana kuiacha. Lakini mtu ambaye anaweza kuachilia mbali tabia au mwenendo popote anapotaka, kamwe hawezi kutawaliwa nao. Mtu anayeacha furaha zote za mwili ambazo mara kwa mara zinamvutia kwenye dhambi,kwa mwezi mzima ili apate radhi ya Mwenyezi Mungu, na anajifunza kujitawala na kujizuia,anaweza kuyashinda kwa mwezi mzima ili apate radhi ya Mwenyezi Mungu, na anajifunza kujitawala na kujizuia, anaweza kuyashinda kwa urahisi majaribio ya kutenda dhambi.

(4) Tena, kama ilivyo katika mwezi wa kufunga Saumu, mtu yampasa kuamka katika saa za mwisho wa usiku kwa kula daku, hapo anapata nafasi zaidi ya kuomba na kuabudu, ambayo humwongoza upesi kwenye njia ya maendeleo ya kiroho, na anapoitoa starehe na faraja yake sadaka kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu anaitia nguvu roho yake na kumvuta awe karibu naye.baki ya Saumu ya mwezi mzima wa Ramadhani ambayo ni ya lazima, mtu anaweza pia kufunga Saumu katika siku zingine.

Kufunga siku ya Ijumaa peke yake, imekatazwa, isipokuwamtu afunge Ijumaa na Jumamosi, au Alhamisi na Ijumaa. Kadhalika kufunga siku za Idi imekatazwa. Mtume Swallalahu alyhi wasallam alisema, “Mtu anayefunga Ramadhani, kisha akafunga siku sita za mwezi wa Shawwaal (Mfunguo mosi), yeye ni kama amefunga mwaka mzima” (Muslim). Kadhalika Mtume Swallalahu alyhi wasallamakasema, “Mtu anayefunga siku moja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi Mungu atamuwekambali na Moto kwa umbali wa miaka sabini” (Muslim). Baadhi ya Saumu zilizo sunna ni kufungasiku ya Arafa, yaani tarehe 9 Mfunguo tatu, na kufunga siku tatu katika kila mwezi.watoto wadogo hawaruhusiwi kufunga.

Kadhalika si ruhusa kwa mtu kufunga siku zote bila kuacha. Mtume swallalahu alyhi wasallam. akasema, “Kwa hakika mimi ni mchaji zaidi kuliko ninyi, lakini wakatimwingine nafunga na wakati mwingine sifungi, basi nanyi mfanye hivyo”. (Bukhari).

Picha/afp

Muumini wa Kiislamu akiisoma Qur’an awali katika Msikiti akisubiri wakati wa Swala. Usomaji Qur’an ni mojawapo wa amali njema kwa Mwislamu wakati wa Ramadhani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.