Wabunge waapa kupinga juhudi za kuhalalisha ushoga

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti -

Na WINNIE ATIENO

WABUNGE wamesisitiza kuwa serikali ya Kenya haitaruhusu mapenzi ya watu wa jinsia moja nchini.

Akiongea kwenye mkutano katika hoteli ya Serena Beach, Kaunti ya Mombasa, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu habari, mawasiliano na teknolojia Bw William Kisang, alisisitiza kuwa mapenzi ya jinsia moja ni haramu Kenya.

“Katiba iko bayana kuhusiana na masuala haya. Nyote mnajua mapenzi ya jinsia moja ni haramu na hatuhitaji sheria nyingine,” alisema Bw Kisang ambaye pia ni mbunge wa Marakwet Magharibi.

Kamati hiyo ilimpongeza mwenyekiti wa bodi ya kudhibiti filamu nchini Ezekiel Mutua katika harakati zake za kuhakikisha kuna maadili nchini hasa kwenye vipindi vinavyopeperushwa kupitia vyombo vya habari.

“Tunaunga juhudi za bodi ya kudhibiti filamu nchini katika kuhakikisha filamu za humu nchini zinafuata maadili ya jamii ya Kiafrika” akasema Bw Kisang.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.