Kipusa akemea jombi kujua alitaka tunda tu

Taifa Leo - - Dondoo! -

KIDOSHO mmoja eneo hili alimfokea mpenzi wake alipopata habari kwamba aliambia marafiki nia yake ilikuwa kuramba asali tu na wala hakuwa na mpango wa kumuoa.

Inaarifiwa wawili hao walianza uhusiano wiki chache zilizopita na juzi kitumbua kikaingia mchanga. Siku ya kisanga, mwanadada alienda katika chumba cha jombi akihema ajabu.

Alipowasili, jamaa alitaka kumkaribisha kwa busu kama kawaida lakini binti aliachilia cheche za maneno. “Nilikupa penzi lakini ukaamua kuniaibisha mtaani. Ulinukuliwa ukisema huna haja nami bali unataka tu kula tunda kisha unitupe," kipusa alimkemea jamaa. Jombi alitaka kujitetea lakini demu hakumsikiza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.