Afichua mapenzi yake kwa mke wa mhubiri

Taifa Leo - - Dondoo! - Na HOLINESS MWAMBI

JOMBI mmoja wa hapa aliwashangaza marafiki alipodai alikuwa akimmezea mate mke wa pasta. Duru ziliarifu kuwa jombi alifichulia marafiki kwamba aliokoka kwa sababu alitaka apate nafasi ya kumnyemelea mke wa mhubiri.

Bila kuona haya, jamaa alidai alikuwa akimtamani mke wa mchungaji kwa siku nyingi.“wacha leo niseme ukweli moyo wangu upone. Nampenda sana mke wa pasta na nataka awe mpenzi wangu," jombi alisema bila kuogopa.marafiki wake walishtuka na kudhani jamaa alikuwa amepagawa lakini akasitiza huo ulikuwa ukweli wa moyo wake. Walimwambia alikuwa amesakamwa na mapepo hatari ya uasherati na alihitaji maombi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.