Hali itakuwa bora kwa mwananchi ikiwa tu ushuru utatumiwa vyema

Taifa Leo - - Barua -

KWA sasa maisha ya mwananchi yako katika hali ngumu mno kwa kuwa lazima atie nguvu zaidi kutafutia familia yake riziki baada ya kuongezwa kwa ushuru.

Bidii na juhudi za mwananchi huenda zisivune chochote ikiwa serikali haitatumia fedha hizo vizuri.

Kwanza serikali inafaa kulipa madeni tuliyo nayo kwa kuwa yametuzonga na kusababisha hali mbaya ya uchumi.

Viongozi wetu wawajibike wasije wakaingiwa na ufisadi na hivyo kuiba hela zinazokusanywa.

Ikiwa mtu yeyote atajaribu kuiba basi achukuliwe hatua kali bila kujali cheo chake au kabila lake.

Nina imani kuwa ikiwa madeni yatalipwa hatutakuwa tena watumwa. Tutaweza kujitegemea kama taifa pasi kuomba misaada kutoka ughaibuni.

HILLARY FLETCHER WANYONYI, Chuo Kikuu cha Egerton.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.