Ujumbe Mfupi

Taifa Leo - - Barua -

MAONI: Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na visa kadha vya mauaji ya wanawake kutokana na mizozo ya kimapenzi. Unadhani nini kinachangia hali hiyo na ni jinsi gani unyama huo unaweza kukomeshwa

Zamani walimu walikua wakiadhibu watoto kwa viboko na wazazi pia wanawatia adabu ya viboko hakukuwa na visa vya vijana kujipata katika mapenzi ambayo baadaye hugeuka kuwa sumu.

Kupitia SMS

Vijana hawana adabu siku hizi, wanatembea nusu uchi na wazazi wamekuwa dhaifu hawawezi kuuliza watoto wao wanapochelewa kufika nyumbani. Wazazi ndio wanachangia katika masaibu haya yanayopata binti zetu mikononi mwa wanaume wakatili.

Kupitia SMS

Kweli kifo cha Sharon, hapa kenya kimeleta hamaki na kuwaacha wengi na maswali kemkem. Wengi wamemshutumu kwamba alikuwa mbaya lakini kwa sababu amefariki hawezi kuelezea ukweli. Hata hivyo mauaji haya ya kiholela yanafaa kukemewa na serikali iingilie kati na kukabiliana na watu wanaotekeleza unyama huo.

Mzee Charo, Embu

Bila shaka jambo linachongia mauaji ya wanawake kutokana na mivutano ya kimapenzi ni wanaume kutoweza kustahimili kuwa na mwanamke mmoja katika ndoa au kwenye uhusiano wa kimapenzi. Tamaa ya pesa za haraka pia inachangia binti zetu kujitia taabuni. Hata hivyo mauaji hayo hayana budi kushutumiwa vikali.

Shebe Zipingoni

Mapenzi ni kama asali na yakibadilika yanakuwa sumu. Kama upendo unaisha, chuki inatokea na mauji yanafuata. Njia ya kipekee ya kukomesha mauji ya kimapenzi ni kuheshimu ndoa na kukomesha tamaa ya utajiri wa haraka.

Kyanzi, Malili

MJADALA WA LEO:

Viongozi kutoka maeneo ya Pwani, wakiwemo wabunge zaidi ya 20, wametangaza kuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto katika uchaguzi wa 2022. Je, unadhani viongozi hao watasimama na Bw Ruto hadi 2022 au watabadili msimamo wao?

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.