Gabriel kumfanya demu Ludmilla wake wa halali

Taifa Leo - - Dimba - The Sun Instagram. The Sun,

FOWADI matata wa Manchester City, Gabriel Jesus amefichua kwamba ndiye anayechovya asali mzingani mwa kichuna Ludimilla Oliveira da Silva japo mwanamuziki huyo mzawa wa Brazil alitaka sana uhusiano wake wa kimapenzi na Gabriel, 21, uwe wa siri.

Ludmilla mwenye umri wa miaka 23 ni mtunzi maarufu wa nyimbo ambaye anastahiwa pakubwa ndani na nje ya Brazil kwa upekee wa sauti yake katika majukwaa ya sanaa ya muziki.

Kwa mujibu wa gazeti la kipusa huyo alianza kutoka kimapenzi na Gabriel kuanzia Julai 2018. Hata hivyo, Ludmilla aliyakana kabisa madai hayo mwishoni mwa wiki jana alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha ‘Coversa com Bial’ cha runinga ya Globo TV, Brazil.

"Hizo ni tetesi ambazo sielewi chanzo chake. Zimeanzishwa mitandaoni na watu wasio na nia nzuri kwa uhusiano wangu na Gabriel ambaye ni rafiki tu wa karibu. Hakuna lolote la mno kati yetu, ila nijualo ni kuwa Gabril ni mtu mzuri na wa kutamanika mno," akaongeza.

Mbali na Gabriel kuanika maazimio ya kumvisha Ludmilla pete ya uchumba mwezi ujao, mama ya kidosho huyo, Silvana Oliveira amefichua pia mpango wa kuolewa kwa mwanawe na Gabriel mwishoni mwa mwaka huu katika harusi ya kukata na shoka.

Kulingana na Ricardo Pipo ambaye ni rafiki wa karibu wa Gabriel, mwanasoka huyo alianza kulimenya tunda la Ludmilla pindi baada ya kufahamiana katika hafla moja iliyowakutanisha jijini Sao

Paulo, Brazil mnamo Julai 22, 2018.

Gazeti la linadai kwamba Ludmilla alikumbatiana na Gabriel mara nyingi mwishoni mwa hafla hiyo na tangu wakati huo, walianza kubadilishana jumbe za kimapenzi na kupanga mikutano ya mara kwa mara katika maeneo ya starehe.

Kulingana na Vera Lucia ambaye ni mamaye Gabriel, yeye alifahamu kuhusu uhusiano kati ya mwanawe na Ludmilla kupitia picha zilizokuwa zikipakiwa na kichuna huyo kwenye mtandao wake wa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.