DUH! MANULA AJUTA KUIFAHAMU SIMBA

Bingwa - - HABARI /TANGAZO - NA HUSSEIN OMAR

MLINDA mlango wa Simba, Aishi Manula, jana alikiona cha moto kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, baada ya kuhenyeshwa na kocha wao wa makipa, Mwarami Mohamed ‘Shilton’.

Wakati kikosi cha timu hiyo kikiwa kinajiandaa na mchezo wao wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Jumapili katika Uwanja wa Uhuru, kocha wa timu hiyo, Joseph Omog, alikuwa akiendelea na programu za kikosi chake hicho.

Kwa upande wa makipa ndio kulikuwa na balaa la aina yake, ambapo Mwarami alikuwa akiwapa mazoezi makali akina Manula na wenzake Denis Richard na Emanuel Mseja.

Manula alionekana kuelewa vizuri mazoezi hayo magumu, lakini yalimhenyesha kiasi cha kulala chali kila mara.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.