Washindi wa michezo ya kubahatisha kukatwa kodi

Bingwa - - HABARI /TANGAZO - NA FERDNANDA MBAMILA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeanza kutekeleza jukumu la kukusanya kodi katika michezo ya kubahatisha tangu ilipokabidhiwa jukumu hilo Julai mosi, mwaka huu kwa mwaka wa fedha wa 2017/18.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo, alisema mpango wa mlipa kodi hapo awali ulikua haupo katika sheria na taratibu za ulipaji kodi katika mamlaka.

Alisema awali mapato yaliyokuwa yakilipwa hayapitii katika mamlaka, hivyo kutokana na maoni ya wananchi wakaona ni vyema kuwapo kwa sheria ambayo itafuatwa katika ulipaji wa kodi.

Alisema bodi ya michezo ya kubahatisha itaendelea kuwa msimamizi wa michezo hiyo nchini kwa mujibu wa sheria na mdau mkubwa katika jukumu la kuratibu michezo ya bahati nasibu.

Aidha, mabadiliko hayo yalikuja kutokana na ukusanywaji wa mapato TRA katika michezo yote ya kubahatisha ambayo ni pamoja na kwenye Casino, Sports Betting, Slot Machines, Lottery na kupitia ujumbe mfupi wa simu (sms).

“Kwa washindi wa mchezo wa kubahatisha tunapenda wafahamu kuwa mshindi katika bahati nasibu atakatwa asilimia 18 ya kiasi alichoshinda,” alisema Kayombo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.