Nonga kukaa nje wiki mbili

Bingwa - - HABARI /TANGAZO - NA WINFRIDA MTOI

MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Paul Nonga, amesema anajisikia vibaya kuikosa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya nyama za paja.

Mwadui iliyopoteza mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, itavaana na Simba kwenye mchezo huo wa raundi ya tatu utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Nonga alisema alipata majeruhi hayo kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar na atakuwa nje kwa wiki mbili.

Alisema alitaka kuwamo kwenye mechi hiyo ili aongeze idadi ya mabao kwa sababu amepania kuwa mmoja wa vinara wa mabao msimu huu wa Ligi Kuu.

“Kwa kweli imeniuma kuikosa mechi ya Simba kwa kuwa nilikuwa nimeipania. Nina bao moja tu hadi sasa nililofunga dhidi ya Singida United, nilitaka kuongeza idadi hiyo kutimiza lengo langu la kufunga mabao mengi msimu huu,” alisema Nonga.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.