Mayanja awakingia kifua washambuliaji

Bingwa - - HABARI /TANGAZO - NA ZAITUNI KIBWANA

KOCHA msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ameitetea safu ya ushambuliaji ya Simba, baada ya mashabiki wa timu hiyo kulalamikia ubutu wao.

Mashabiki wa Simba wamekuwa wakilalamikia safu yao ya ushambuliaji kushindwa kufunga kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam.

Mayanja, ambaye anasaidiana na Joseph Omog kukinoa kikosi hicho, alisema safu yao ya ushambuliaji kila siku inafanyiwa kazi hivyo ni jambo la kuwapa muda.

“Tunaifanyia kazi safu ya ushambuliaji, hivyo wachezaji wanapaswa kupewa muda,” alisema Mayanja.

Akizungumzia maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC itakayochezwa Jumapili wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru, alisema: “Tunaendelea na mazoezi na tuna imani tutaweza kufanya vema kwenye mchezo huo.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.