OKWI

ATUMIKA MIKAKATI YA UBINGWA

Bingwa - - MBELE - Tanzania Bara.

KOCHA Mkuu wa Simba Mcameroon, Joseph Omog, amewapa majukumu mazito nyota wake, akiwamo Emmanuel Okwi, kuhakikisha wanafanya kila liwezekanalo kupata ushindi katika mechi zao zijazo za Ligi Kuu

Japo safu zote za timu hiyo zina nafasi sawa katika kusaka ushindi, Omog anaamini kuwa, hilo litawezekana iwapo ile ya ushambuliaji itatimiza majukumu yake ipasavyo ya kuzifumania nyavu. Katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Simba ilishindwa kupata bao na mchezo kumalizika kwa suluhu, japo safu nyingine, yaani ulinzi na ushambuliaji, zilicheza vizuri mno.

Ni kutokana na hali hiyo, amewataka washambuliaji wake wa kati, Okwi, John Bocco na Nicholas Gyan kuhakikisha kila mechi wanaibuka na ushindi wa mabao matatu na kuendelea katika michezo ya Ligi Kuu Bara.

Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba kumpa masharti Mcameroon huyo kuhakikisha anashinda mechi tano mfululizo, wakianzia mechi na Azam yaliyotoka suluhu ambapo asipofanya hivyo, huenda kibarua chake kikaota nyasi.

Omog ameanza kuhakikisha vijana wake hawamuangushi kwa kuwapa majukumu ya kuhakikisha wanafanya mauaji kuanzia katika mchezo wao ujao dhidi ya Mwadui FC, utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini.

Akizungumza na BINGWA jijini jana, Omog alisema baada ya kutoka suluhu na Azam, ameanza kutoa majukumu kwa safu yake ya ushambuliaji, akiwataka kila mechi kuibuka na ushindi wa mabao matatu na kuendelea.

“Hilo wanalitambua kwamba kwa sasa tunahitaji ushindi wa idadi kubwa ya mabao, tunaanzia katika mechi yetu dhidi ya Mwadui, tunahitaji kupata ushindi wa mabao mengi ili tuweze kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo,” alisema.

Hilo wanalitambua kwamba kwa sasa tunahitaji ushindi wa idadi kubwa ya mabao, tunaanzia katika mechi yetu dhidi ya Mwadui.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.