Tanzania yashuka nafasi 5 Fifa

Bingwa - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

TANZANIA imeendelea kusota kwenye viwango vya soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), baada ya kuporomoka kwa nafasi tano.

Ripoti ya Fifa iliyotoka jana inaonyesha kwamba, Tanzania imejikusanyia pointi 256, hivyo kushika nafasi ya 125 kutoka 120 iliyokuwa awali.

Katika ripoti iliyopita, Tanzania ilipanda kutoka nafasi ya 144 hadi 120, hivyo hii ya juzi ni mwendelezo wa mwenendo wake mbovu kwenye maendeleo ya mchezo wa soka.

Lakini kushuka kwa Tanzania kwenye ripoti mpya ni wazi hali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kitendo cha Taifa Stars kutofuzu fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan), michuano itakayofanyika mwakani nchini Kenya.

Kwa upande wao Kenya nao wameporomoka kutoka nafasi ya 82 waliyokuwa mwezi uliopita hadi 88, kwa maana kwamba wameshuka kwa nafasi sita.

Lakini pia, mambo yameendelea kuwa mazuri kwa Uganda waliopanda hadi nafasi ya 71, wakipanda nafasi mbili kutoka 73 waliyokuwa mwanzoni, mafanikio yaliyochangiwa na matokeo mazuri katika michezo yao ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani nchini Urusi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.