Azam kulipa kisasi kwa Kagera Sugar

Bingwa - - HABARI - NA WINFRIDA MTOI

TIMU ya Azam FC inatarajia kushuka dimbani leo kwenye uwanja wao wa Azam Complex, Dar es Salaam, katika mchezo wa raundi ya tatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Wiki iliyopita Azam walikutana na Simba katika uwanja huo na kutoka suluhu, lakini pia itakutana na Kagera Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 kwenye uwanja huo.

Bao hilo pekee lilifungwa na Themi Felix, katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo na kuwaondoa Azam katika nafasi ya tatu waliyokuwa wanashikilia.

Hata hivyo, leo huenda Azam FC wakampa kazi maalumu mshambuliaji wake, Mbaraka Yusuf, kulipa kisasi kwa Kagera Sugar waliyemsajili kutoka kikosi hicho kinachonolewa na Mecky Mexime.

Yusuf ni miongoni mwa wachezaji aliyeisumbua safu ya ulinzi ya Azam siku hiyo, lakini hivi sasa ni mali ya Wanalambalamba hao.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha msaidizi wa timu hiyo, Idd Cheche, alisema lengo lao kubwa ni kushinda mchezo huo hivyo watapanga kikosi imara kitakachosaidia kupata matokeo chanya. Alieleza kuwa msimu huu wamekuja kivingine na malengo yao ni ubingwa, hivyo michezo ya nyumbani kwao ni muhimu katika kuhakikisha wanapata pointi kwa kila mechi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.