Mwambusi aitwa Mbeya City

Bingwa - - HABARI - NA ZAINAB IDDY

BAADA ya siku moja tu kupita tangu uongozi wa Mbeya City kuamua kuvunja mkataba na kocha Kinnah Phiri, aliyewahi kuwa kocha katika kikosi hicho, Juma Mwambusi, ameitwa kukinoa kikosi hicho.

Juzi mchana uongozi wa Mbeya City walikutana na kocha Mmalawi, Phiri, baada ya kupokea agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala, juu ya kuzungumza naye kuhusu hatima yake ndani ya timu hiyo.

Tangu kuanza msimu huu, Phiri hajakaa kwenye benchi la ufundi na majukumu hayo amepewa kocha msaidizi, Mohamed Kijuso.

Akizungumza na BINGWA, Kijuso alisema kwa kuwa hivi sasa kocha mkuu hayupo, mtu anayeweza kuipa mafanikio Mbeya City ni Mwambusi pekee ambaye alishawahi kufanya kazi nao. “Binafsi namkubali Mwambusi na kama itatokea atarejea kuja kufanya kazi Mbeya City, sina shaka msimu huu utakuwa na mafanikio kwetu.

“Licha ya kupenda na kufurahishwa iwapo kama Mwambusi atarejea, lakini mwisho wa siku uongozi ndio wenye uwezo wa kuamua nani aje kufundisha hivyo siwezi kuamua hilo,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.