Matola avuliwa ukocha mkuu Lipuli

Bingwa - - HABARI - NA JESSCA NANGAWE

UONGOZI wa klabu ya Lipuli FC, umemshusha cheo kocha wake mkuu, Selemani Matola na kumpa nafasi hiyo kocha wa zamani wa Simba, Amri Said, kushika nafasi hiyo.

Matola amenyang’anywa cheo hicho baada ya kukosa sifa za kufundisha, kutokana na kuendelea kumiliki leseni C ambayo haimpi kibali cha kufundisha.

Akizungumza na BINGWA, Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo, Benedict Kiwelo, alisema kwa sasa Matola atatambulika kama kocha msaidizi huku nafasi yake ikishikiliwa na Amri Said hadi hapo atakapokua na sifa za kuwa kocha mkuu.

“Matola ataendelea kuwa na sisi lakini atatambulika kama kocha msaidizi, tulikua tunatambua kuwa ana leseni C toka awali na yupo kwenye mchakato wa kujiendeleza ili awe na sifa za ukocha mkuu, tunategemea tutaendelea kupata ushirikiano wake kama mwanzo,” alisema Kiwelo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.