DC Nachingwea amkabidhi milioni 50 mshindi Biko

Bingwa - - STORI ZA KITAA - NA MWANDISHI WETU, NACHINGWEA

MKUU wa Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, Rukia Muwango, amemkabidhi Sh milioni 50 mshindi wa Biko wa droo ya 40, Norbert Litimba, katika mchezo wa bahati nasibu ya Watanzania.

Rukia alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana Tawi la Benki ya NMB mjini Nachingwea, ikiwa ni siku moja baada ya mkazi huyo wa Nachingwea kuvuna mamilioni hayo ya Biko.

DC Rukia alimpongeza Litimba na kumkumbusha namna bora ya kukuza uchumi wake kwa kupitia sekta nzuri ya michezo ya kubahatisha nchini Tanzania, ikiwamo Biko.

"Najivunia sana wewe mwananchi wangu wa Nachingwea kuwa mmoja kati ya wengi wanaotangazwa kushinda zawadi kubwa za Biko tangu kuanzishwa kwa mchezo huu hapa nchini, hivyo nashauri wengine wajitokeze kuwania mamilioni haya," alisema.

Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema gurudumu la Biko la kumwaga zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na milioni moja linaendelea bila kusahau zawadi kubwa ya Sh milioni 50 inayotoka kila Jumatano na Jumapili.

"Zawadi za papo kwa hapo zinatoka kila baada ya dakika moja bila kusahau donge nono la Sh milioni 50, hivyo Watanzania waendelee kucheza kwa wingi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kushinda zawadi zetu, ukingatia kuwa mchezo wetu unatumia ujumbe wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money, ambapo namba ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456, huku tiketi moja ikipatikana kwa Sh 1,000 na kuendelea," alisema Melles.

Kwa upande wake, Litimba aliwashukuru Biko kwa kuyabadilisha maisha yake kwa kumtangaza mshindi sanjari na kumkabidhi fedha zake bila usumbufu wowote.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.