Ligi ya wanawake mechi mbili mabao 38

Bingwa - - STORI ZA KITAA - NA MASYENENE DAMIAN, MWANZA

LIGI ya soka ya wanawake mkoani hapa imetia fora baada ya kushuhudia mabao 38 yakifungwa katika mechi zilizochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Alliance na TSC Academy zinaongoza kwa kutoa vipigo vya mbwa mwizi kwa wapinzani wao katika ligi hiyo, inayoshirikisha timu nne za mkoani hapa.

Katika mchezo uliochezwa juzi, timu ya TSC Academy iliibuka na ushindi mnono wa mabao 12-0 dhidi ya JB FC.

Mabao ya washindi hao yalifungwa na Khamisa Kassim, Asteria Robert, Paulina Christopher, Yasinta Peter na Merabu James.

Katika mchezo mwingine, timu ya Alliance iliibuka na ushindi wa mabao 26-0 dhidi ya Nyanguge Kombaini.

Mabao ya Alliance yalifungwa na Enekia Kasonge, Asnath Linus, Sharifa Anidu, Mwamvita Tabago, Esther Mabanza, Aisha Edward, Janeth Matulanga na Elizabeth Edward.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.