JICA waleta neema riadha

Bingwa - - STORI ZA KITAA - NA GLORY MLAY

SHIRIKA la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA), kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limeandaa mashindano ya riadha kwa wanawake yatakayofanyika Novemba 25-26, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA juzi, Ofisa Michezo wa BMT, Benson Chacha, alisema mashindano hayo yatawezesha kuwapata wanariadha bora.

Chacha alisema wanariadha watakaoonyesha viwango katika mashindano hayo wataweza kuchaguliwa kwenye kikosi cha Taifa kwa michuano ya kimataifa.

“Mashindano hayo yataibua vipaji vya wanariadha wanawake watakaopata nafasi ya kuunda timu ya taifa itakayoshiriki michuano ya kimataifa, ikiwamo ile ya Olimpiki, itakayofanyika 2020,” alisema.

Alisema wanariadha 155 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Chacha alisema kila mkoa utatoa wanariadha watano ili kushiriki mashindano hayo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.