TUMUACHE RONALDO NA UEFA YAKE

Bingwa - - SPORTS -

KWA lugha nyingine unaweza kusema tumuache straika Cristiano Ronaldo na Ligi ya Mabingwa yake.

Usemi huu unatokana na maajabu ambayo amekuwa akiyafanya na kumwezesha kuweka rekodi katika mashindano mbalimbali.

Jambo hilo alilidhihirisha usiku wa kuamkia jana, wakati nyota yake ilipozidi kung’ara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo, Ronaldo ndiye aliyeibuka shujaa kwa kuweza kufunga mabao mawili kati ya matatu ambayo yaliiwezesha Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya APOEL, katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi.

Kwa kufunga mabao hayo, kumemfanya CR7 kuweka rekodi nyingine kati ya anazozishikilia katika michuano hiyo.

Katika Makala haya, BINGWA imejaribu kuangalia jinsi nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Ureno alivyozidi kufunika katika michuano hiyo.

Kwa kupachika mabao hayo, Ronaldo atakuwa amemfunika tena hasimu wake, Lionel Messi, kwa kucheka na nyavu katika michuano hiyo mikubwa Ulaya kwa njia ya mikwaju ya penalti.

Hii ni kutokana na kwamba Ronaldo atakuwa amefikisha mabao 12 dhidi ya Messi, ambaye hadi sasa amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 11 kwa njia hiyo.

Mbali na hilo, pia idadi hiyo imemfanya ampite tena Messi kwa kufunga mabao mengi katika michuano hiyo akiwa nyumbani, ambapo hadi sasa Ronaldo ameshafunga 55 dhidi ya 54 aliyofunga akiwa kwenye Uwanja wa Camp Nou akiwa na klabu yake ya Barcelona.

Idadi hiyo pia imemfanya Ronaldo kuifungia Real Madrid mabao 12 katika michezo 16 katika mashindano yote na huku akiwa amewafungia mabingwa hao wa Hispania na Ulaya bao katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo katika kipindi cha misimu sita na ndiye amekuwa akifunga bao la kwanza.

Pia idadi hiyo imemfanya staa huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno, sasa kufikisha mabao 107, ambayo ni zaidi ya timu 116 zote zilizowahi kushiriki katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa kufunga mabao hayo, kumemfanya CR7 kuweka rekodi nyingine ka ya anazozishikilia ka ka michuano hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.