Familia ya Heskey yasombwa na kimbunga

Bingwa - - SPORTS -

NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya England na Liverpool, Emile Heskey, amesema baadhi ya wanafamilia wake hawajulikani mahali walipo, baada ya kimbunga Irma kuvikumba visiwa vya Caribbean.

Kimbunga hicho, ambacho kiliambatana na mvua na upepo mkali, kilivikumba visiwa hivyo wiki iliyopita na kuharibu asilimia 95 ya majengo yote yaliyopo katika kisiwa cha Barbuda.

Akizungumza juzi, Heskey alisema kuwa, wazazi wake wapo salama katika kisiwa cha Antigua, lakini bado hajapata taarifa kamili kwa muda wa wiki nzima kuhusu ndugu zake wanaoishi katika kisiwa cha Barbuda.

"Mama yangu hajaweza kuzungumza nao," straika huyo wa zamani aliiambia BBC News. "Baba na mama wana bahati hawakuweza kukumbwa na gharika hili, lakini familia ya mama iliyopo katika kisiwa cha Barbuda wamesombwa na kimbunga na kila kitu kimeteketea,” aliongeza staa huyo wa zamani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.