Jamie Vardy aimarisha ulinzi nyumbani kwake

Bingwa - - SPORTS -

STRAIKA wa Leicester City, Jamie Vardy, anaripotiwa kuongeza vifaa vya ulinzi nyumbani kwake, baada ya yeye na mkewe, Rebekah, kupokea ujumbe wenye vitisho vya kuuawa.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, staa huyo amechukua hatua hiyo juzi, ikiwa ni baada ya kuhamia katika makazi mengine mapya yaliyopo eneo la Lincolnshire, baada ya yale ya awali kuoneshwa hadharani.

Gazeti hilo lilieleza kwamba, katika kuimarisha ulinzi huo, staa huyo wa timu ya taifa ya England amefunga kamera katika kila chumba, ikiwa ni baada ya kupokea ujumbe huo ambao ulikuwa umemlenga mkewe.

Kutokana na hali hiyo, kwa sasa Vardy anaweza kutembea ndani na nje ya jengo hilo kwa kutumia msaada wa simu yake ya mkononi ambayo imeunganishwa na kamera hizo kali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.